JEE HUU NI UNGWANA?
Tuka safiri kutoka inchi yetu kuu ya Kenya, tukaja hapa ulaya na tukayafanya hii makao yetu. Wengi wetu tumefanikiwa tuna makaratasi sisi ni wananchi hapa ngambo Kazi tunafanya bila shida na hata biashara tumefungua. Kusema biashara si kuuza maharagwe ni ati zile ‘Security Agency’ tumefungua, ati sasa tunaweza kuwasaidia wakenya wenzetu. Naskia fununu ati walio fanikiwa wakaweza kupata zile contract za kazi kutoka kwa serikali ya hapa wanalipwa ‘mbao’(LL’s) kadhaa....... kitu kama ‘mbao’ kumi na nne hivii alafu tuna waandika wakenya wenzetu kazi ambao hawana mkaratasi kwa jina ya kuwasaidia alafu wana walipa ‘mbao’ tatu au nne. ‘Jee huu ni unguana?????!!!!! Usisahau mkenya mwenzangu..... Kile unacho panda ndicho utakacho vuna.
Ewe Mola tuepushe na mahasidi
Katika mkoa wa Miltonkeynes naskia dada wetu alianga dunia lakini kile aliacha waKenya wenzangu tulishangaa. Dada huyu alikua amejibebea chungu nzima. Wazee niko na swali, mama mkenya akipiga simu aseme, ‘Baba Jane niko shidani, pipes zangu kavunjika maji yamejaa nyumba’ au ‘ motokaa yangu kataa kuanza’ utaenda?
Siku ingine wazee think twice because u might get there and the lady has set a trap for u. Sasa huyu dada aliacha video na majina ya wazee karibu ishirini, kwake wamelala na tendo likafanyika. Dada wetu alijua uko HIV+. Sasa wakenya huu ni ugwana kweli? Nawauliza?

Read more